Ukitaka kuishi, lazima uwe na nguvu na akili
Hapo zamani za kale, kulikuwa na marafiki wa karibu: Bw. Chuma, Bw. Kioo na Bw. Achari. Bw. Chuma alitengenezwa kwa chuma, Bw. Kioo alitengenezwa kwa kioo, na Bw. Achari alitengenezwa kwa achari. Walikuwa watu maskini wasioweza kufanya kazi, na waliishi katika kibanda kidogo kando ya jumba kubwa la zimwi.
Walikwenda jikoni kwa zimwi wakala, kisha wakarudi kwenye kibanda chao kidogo. Lakini siku moja walipokuwa wakila, mke wa zimwi aliwaona jikoni. Alikasirika, akawaambia wasije tena hapo.

Siku iliyofuata walirudi na kuanza kula jikoni, lakini aliwaona, na safari hii alikuwa amekasirika kweli. Walikimbia, naye akawafuata, na safari hii alimkamata Bw. Kioo na kumpuliza. Bw. Kioo akapaa hewani, akaanguka chini, akavunjika vipande vipande na kufa. Marafiki zake walihuzunika, lakini hawakuweza kumfanyia chochote.

Siku iliyofuata, Bw. Chuma na Bw. Achari walirudi tena na kuanza kula, lakini yeye aliwafuata tena. Walikimbia, naye akawafuata, na safari hii alimkamata Bw. Achari, kisha akampuliza. Akapaa hewani na kuanguka chini, kisha akakatika na kufa. Bw. Chuma alihuzunika sana na kukasirika, na alitaka kulipiza kisasi.

Siku iliyofuata, Bw. Chuma alikwenda jikoni kwa zimwi na kuanza kula. Mke wa zimwi alimwona na kumuuliza kama anataka kufa kama marafiki zake. Bw. Chuma alisema hawezi kumuua, kisha akampuliza, na Bw. Chuma akapaa hewani na kuanguka chini, lakini hakufa kwa sababu alitengenezwa kwa chuma. Kwa hiyo alipuliza kwa nguvu zaidi kuliko mara ya kwanza, lakini bado hakufa. Alijaribu tena, lakini safari hii alipokuwa akimpuliza, mdomo wake ulipasuka, na Bw. Chuma akamcheka.

Alikwenda kwa fundi cherehani ili kushonwa mdomo wake uungane tena. Baadaye alikwenda kwenye kibanda kidogo cha Bw. Chuma na kumwita: "Njoo huku kama wewe ni mwanaume shupavu!". Bw. Chuma alitoka kwenye kibanda chake kidogo, naye akajaribu kumpuliza, lakini mdomo wake ulipasuka tena. Bw. Chuma akamcheka. Alikasirika sana, kisha akaenda tena kwa fundi cherehani kushonwa mdomo wake.


Kwa kuwa hakuweza kumuua, aliamua kumnasa atakapokuja jikoni kwake. Siku iliyofuata, Bw. Chuma alikwenda jikoni, lakini mke wa zimwi alimkamata, akamweka ndani ya mfuko imara na kuufunga mfuko huo kwa kamba ya mnyongaji. Kisha akamchagua binti yake Memona amlinde Bw. Chuma.

Mke wa zimwi alitaka kumpika Bw. Chuma na kuwaalika ndugu zake wote wamle, kwa hiyo alimwambia binti yake kuwa makini asiufungue mfuko. Kisha akatoka nyumbani kwenda kuwaalika ndugu zake waje kwa chakula cha jioni.
Bw. Chuma alimsikia akisema anataka kumla. Akajiuliza angewezaje kutoka ndani ya mfuko. Akaanza kutafuna chingamu kwa sauti kubwa na kusema "Chingamu nyekundu, mmmm, tamu tamu! Chingamu kijani, mmmm, tamu tamu! Chingamu buluu, mmmm, tamu tamu!", akirudia mara nyingi. Kwa bahati nzuri, binti wa zimwi (Memona) alitamani chingamu, kwa hiyo alimwomba Bw. Chuma ampe kipande.

Bw. Chuma alimwambia hawezi kumpa chingamu kwa sababu mfuko umefungwa. Alimwambia anaweza kutoboa tundu dogo kwenye mfuko, lakini yeye akasema hawezi, kwa sababu mama yake alimwamuru asiufungue mfuko. Hivyo Bw. Chuma alingoja kwa dakika moja, kisha akarudia "Chingamu nyekundu!!! mmmm, tamu tamu! Chingamu kijani!!!! mmmm, tamu tamu! Chingamu buluu!!!!! mmmm, tamu tamu!". Hatimaye akakubali, kwamba atatoboa tundu dogo.
Alitoboa tundu dogo, kisha akasema "Nipe kipande cha chingamu, tafadhali". Lakini Bw. Chuma alimwambia hawezi kutoa chingamu kwa sababu tundu ni dogo mno. Kwa hiyo alilipanua na kumuuliza "Sasa utanipa chingamu, tafadhali?", lakini tena akasema, "Hapana siwezi, tundu halitoshi!". Alilipanua tundu zaidi, lakini Bw. Chuma hakukubali mpaka tundu lilipokuwa kubwa vya kutosha naye akaweza kutoka kupitia humo.

Mke wa zimwi aliporudi na ndugu zake, waliona chakula kimeshawekwa mezani. Mke wa zimwi akasema binti yake ni bora kabisa kwa sababu amempika Bw. Chuma, kwa hiyo wakaanza kula.

Lakini walipomaliza kula, mke wa zimwi alikwenda kwenye jokofu na kufungua friza, akaona kichwa cha binti yake. Alipiga kelele "Hapanaaaaaa!?!????" na kuanza kulia, lakini Bw. Chuma alianza kucheka na kukimbilia juu ya paa la nyumba ya zimwi.
Alimfuata juu ya paa, lakini Bw. Chuma alimdhihaki na kusema "Hiki ni shati la Memona", kisha akamrushia shati hilo. Alikuwa analia kwa uchungu, kisha akasema "Hii ni gauni la Memona", na kumrushia pia. Kisha akasema "Hizi ni chupi za Memona", na kumrushia hizo pia.

Hatimaye Bw. Chuma alikimbilia mahali mbali, akiwa ameridhika kwamba alilipiza kisasi cha vifo vya marafiki zake, na mke wa zimwi amepoteza kila alichokipenda.
Funzo la hadithi hii ni:
